Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Bara ndugu Amani Golugwa ameendelea leo kutoa ushahidi wake wa utetezi dhidi ya Tundu Lissu huku akiweka mkazo wenye msisitizo kwamba tuhuma zinazomkabili Mwenyekiti wao ni tuhuma za uongo na zimelenga kudhoofisha Operesheni ya chama hicho ya No Reforms No Elections ambayo ilikua ikiendelea nchi nzima.

Golugwa ambaye ni shahidi wa tatu wa utetezi aliyeanza kutoa ushahidi wake jana Septemba 2,2025, ameyasema hayo leo Septemba 3,2025 kwenye ushahidi wake wa msingi ambapo pamoja na mambo mengine ameeleza kuwa hata maneno yaliyotumika kumshtaki Lissu kwenye hati ya mashtaka hayafanyi kuwa kosa la Uhaini.
Lissu ambaye ni Mwanasiasa mashughuli wa Upinzani na mkosoaji mkubwa wa Serikali ya Tanzania, anakabiliwa na kesi ya uhaini akidaiwa kutenda kosa la kuitishia Serikali, kinyume na kifungu cha 39(2) (d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu (Penal Code – PC) Rekebu ya mwaka 2023.
Anadaiwa kuwa Aprili 3, 2025, akiwa raia wa Tanzania, kwa nia ya uchochezi alishawishi umma kuzuia kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, kwa kutamka na kuandika (kuchapisha) mtandaoni maneno ya kumshinikiza kiongozi Mkuu wa Serikali ya Tanzania.
Maneno hayo yanayodaiwa kuwa ya uhaini, Lissu alitamka kuwa : “Wanasema kitu kimoja hapa, msimamo huu unaashiria uasi, ni kweli…, kwa sababu tunasema tutazuia uchaguzi, tutahamasisha uasi, hivyo ndivyo namna ya kupata mabadiliko…, kwa hiyo tunaenda kikinukisha…, sana sana huu uchaguzi tutaenda kuuvuruga kwelikweli…, tunaenda kukinukisha vibaya sana…”
Golugwa katika ushahidi wake leo wakati akiongozwa na Tundu Lissu amesema hata kuhusiana na tuhuma za kwamba Lissu ndie aliyechapisha maneno kwenye Jambo Tv ni tuhuma za upotoshaji
Hapa ni sehemu ya kilichojiri wakati wa maswali kati mshtakiwa na Shahidi
Lissu: Turudi kwenye Watazamaji walitumia muda wao Kimataifa, watazamaji wote hao walisemaje juu kufunguliwa kwangu kwa kwsi hii ya Uhaini
Golugwa: Kwanza walisikitishwa nanwalisema kesi hii ya uongo na hawakuona mazingira ya Uhaini kwa kile walichokisikia katika maneno aliyoyazungumza Mh Tundu Lissu na hivyo wakataka na kuzisihi mamlaka zimwachilie huru bila masharti yoyote
Lissu:Waeleze Waheshimiwa majaji baraza la haki za binadamu la umoja wa Mataifa limesemaje juu ya kesi hii
Golugwa:Limesema kukamatwa kwangu kwa kwsi Lissu haikua halali na kitendo cha kukamatwa kwake kinaminya uhuru na haki ya kujieleza na shtaka alilofunguliwa ni shtaka katili lenye lengo la kumuumiza na hivyo kutaka mamlaka zimwachilie kwa sababu kesi inaonekana ni ya kisiasa
Lissu: Waeleze Waheshimiwa majaji kikao cha Mawaziri wa Jumuiya ya Madola kinasemaje juu ya kesi hii
Golugwa: Waheshimiwa Majaji kikao cha mawaziri kimesema kwanza kesi hii inadhihirisha umonywaji wa Demokrasia, kesi hii ni ya kisiasa, na ni batili na hivyo Tundu Lissu aachiliwe bila mashart yoyote.
Lissu:Sasa turudi kwenye mkutano wa trh 3 Aprili 2025.Kwenyw ushahidi wako jana ulisema Mkutano huu uliandaliwa na Sekretalieti ya chama kwa wazo la Katibu Mkuu, Waeleze Waheshimiwa majaji watu wengine waliohudhuria
Golugwa :Watu wengine waliohudhuria mkutano huo waliku Ami Viongozi wa chama ambao hawakua watia ni Ana waandishi wa habari walioalikwa
Lissu:Wafafanulie Waheshimiwa majaji ukisema Viongozi wa chana ambao hawakuwa watia nia una maana gani
Golugwa:Ninamaanisha walikuwepo Viongozi wa Chama kwenyw ngazi ya Jimbo, Mkoa na Wilaya
Lissu:Waeleze Waheshimiwa majaji kama Viongozi wa Chama ni hao tu
Golugwa:Waheshimiwa Majaji walikuwepo pia Viongozi wakuu ambao sio watia nia nikiwemo Mimi mwenyewe
Lissu:Shahidi Waeleze Waheshimiwa majaji wote uliowataja walijuaje kuna mkutano
Golugwa: Waheshimiwa majaji nianze na Viongozi wakuu, Mimi ndie niliyefanya jukumu la kuwapigia simu Viongozi wafuatao, Mwenyekiti Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti Bara John Heche, Makamu Mwenyekiti Zanzibar Said Mzee Saidi na Naibu Katibu Mkuu. Hawa niliwapigia simu mimi mwenyewe na kuwaambia kuhusiana na uwepo wa mkutano huo. Wengine waliokuwepo Ukumbuni walialikwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Chama Brenda Rupia ambaye ni mjumbe wa Sekretalieti
Lissu:Waeleze Waheshimiwa majaji wakati yote hayo yanafanyika mimi nilikua wapi
Golugwa:Waheshimiwa majaji wakati haya yote yanafanyika Tundu Lissu alikua kwenye Operesheni ya Chama iliyokuwa inaendelea Kanda ya Nyasa ya No Reforms No Elections.
Lissu:Waeleze Waheshimiwa majaji mimi nilishiriki kwa namna yoyote ile
Golugwa:Waheshimiwa Majaji Tundu Lissu hakushiriki kuanzia kwenye maandalizi ya kikao hiki, na hata katika kuwasiliana na kutuma mialiko kwa hao watia nia
Lissu:Waeleze Waheshimiwa majaji ushiriki wanguu katik kuwaalika waandishi wa habari
Golugwa :Tundu Lissu hakushiriki katika kuwaalika Waandishi wa habari kuja katika mkutano huu
Lissu: Imedaiwa kwenye Mahakma hii kwamba mimi ndie niliyeitisha hao watu kwenye mkutano
Golugwa:Waheshimiwa majaji hayo madai yatakua ya uongo, ya upotoshaji Tundu Lissu hakuhusika
Lissu:Waeleze Waheshimiwa majaji uwepo wa Waandishi wa Habari katika mkutano huo
Golugwa:Walikuwepo waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali, wa Television, Magazeti, Online Television pamoja na Redio
Lissu:Waeleze Waheshimiwa majaji vyombo vya habari vilivyowakikishwa
Golugwa:Kwa kumbukumbu nakumbuka kulikua na Clouds Tv, nakumbuka uwepo wa Jambo Tv, nakumbuka uwepo wa Chanzo TV, ITV na ninakumbuka kuwaona Waandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi
Lissu:Waeleze Waheshimiwa majaji hao waandishi walialikwa na nani
Golugwa:Waheshimiwa majaji walialikwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi Brenda Rupia ambaye ni mjumbe wa Sekretalieti
Lissu:Waeleze Waheshimiwa majaji kwa kumbukumbu zako uwepo wa masharti yoyote waliopewa hao Waandishi wa Habari
Golugwa: Hapakuwa na masharti yoyote ambayo wamepewa
Lissu:Waeleze Waheshimiwa majaji kwa kumbukumbu zako uwepo wa maelekezo kutoka kwangu au kwa kiongozi yoyote juu ya waandishi wa habari juu ya namna ya kufanya kazi
Golugwa:Hapakuwa na maelekezo kutoka kwa Tundu Lissu au kiongozi yoyote yule kwenda kwa Waandishi wa habari kuhusiana na wao kufanya kazi zao
Lissu:Waeleze Waheshimiwa majaji uwepo wa matangzo ya moja kwa mojayaliyofanywa kwenye mkutano huo yaliyofanywa na vyombo vyabhabari
Golugwa:Ni kweli kulikuwa na matangazo ya moja kwa moja
Lissu:Waeleze Waheshimiwa majaji vyombo vya habari vilivyorusha matangazo ya moja kwa moja, kama unavikumbuka
Golugwa: Kwa kumbukumbu zangu waliorusha matangazo ya moja kwa moja ni Jambo Tv na Chanzo Tv
Lissu:Inadaiwa mimi ndiye niliyerusha matangazo hayo kwenye Jambo Tv
Golugwa :Huo ni uongo, sio kweli huo ni upotoshaji
Lissu: Waeleze Waheshimiwa majaji uhusika wangu kwenye kuchapisha maneno yaliyopo kwenye hati ya mashtka kwenye Jambo Tv
Golugwa:Hakuna uhusika wowote kwamba yeye ndiye aliyechapisha maneno hayi kwenye Jambo Tv
Lissu: kwa ufahamu wako maneno haya yalichapishwa na nani kwenye Jambo Tv
Golugwa: Maneno hayo yamechapishwa na Mwandishi wa Habari ambaye tulimualika wa Jambo Tv
Lissu: Kwa hiyo Shahidi hii tuhuma kwamba mimi ndie niliyechapisha maneno haya unaizungumziaje
Golugwa :Hii tuhuma ni uongo ilikua I na nia ya kuzorotesha Operesheni iliyokuwa inaendelea hakuchapisha Tundu Lissu
Lissu:Inadaiwa kwamba nilichapisha hayo maneno kwenye mtandao wa Jambo Tv nikiwa na nia ya kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Waeleze Waheshimiwa majaji kama kuna maneno Serikali ya Jamhuri ya Muungano
Golugwa: Nimeyasikia maneno hapo na mimi nimekuwepo kwenye huo mkutano hakuna neno Serikali ya Jamhuri ya Muungano
Lissu: Waeleze Waheshimiwa majaji katika hayo maneno uwepo wa neno Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Golugwa:Waheshimiwa majaji hilo neno halipo
Lissu:Kwa ufahamu wako mtu akisema msimamo huu msimamo huu unaashiria Uasi anakua ametenda kosa gani
Golugwa :Hakun kosa lolote ambalo atakuwa ametenda kwa ufahamu wangu
Lissu:Kuna maneno yamezungumzwa kwamba trh 29 Oktoba vituo vikechomwa moto, tutaumiza watu, sasa katika maneno niliyokusomea Waeleze Waheshimiwa majaji uwepo wa maneno tutachoma vituo vya mwendokasi
Golugwa:Katika maneno niliyosomewa hakuna neno lolote kwamba tutaenda kuchoma vituo vya mwendokasi hakuna
Lissu:Katika maneno niliyokusomea Waeleze Waheshimiwa majaji uwepo wa maneno tutachoma vituo vya kupigia kura
Golugwa:Hakuna maneno hayo
Lissu:Waeleze Waheshimiwa majaji kwa kumbukumbu zako iwapo ulimsikia Jaji Chande alitaja waliosababisha hivyo vifo
Golugwa :Waheshimiwa kwa kumbukumbu zangu Sikumbuki iwapo aliwataja waliosababisha vifo
Lissu:Waeleze Waheshimiwa majaji juu ya sababu alizozitoa jaji mkuu kuhusu mauaji hayo
Golugwa: Kwa kumbukumbu zangu sababu alizozitoa ni pamoja na madai ya Katiba Mpya, masuala ya utekaji na watu kupotea na manung’uniko oya muda mrefu ya wananchi ambayo hayajakua yametatuliwa.
Kesi inaendelea