Watu watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wanadaiwa kumvamia mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Mudzi(22), majira ya usiku ambapo wamempora mwanamke huyo pesa tasilimu kiasi cha dola 200 za Marekani.
Watu hao mara baada ya kuchukua pesa hizo walimbaka mwanamke huyo kwa zamu na kisha kumpiga mapanga eneo la begani na baada ya kuona mwanamke huyo amepoteza fahamu walikimbia pasipojulikana.
Mudzi ambaye ni raia kutoa nchini Zimbabwe alivamiwa na watu hao nyumbani kwake ambako anaishi mwenywe muda mfupi tu tangu atoke kwenye shughuli zake za kujitafutia pesa.
Msemaji wa Polisi Mkoa wa Mashonaland Mashariki Inspekta Simon Chazovachiyi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema polisi wameanzisha msako wa kuwatafuta washukiwa hao.
Kwa mujibu wa wa Inspekta Simon mwanamke huyo alisalimisha dola 200 za Marekani na simu ya mkononi ya Techno kabla ya watatu hao kuanza kumbaka