Rais wa Marekani,Joe Biden anashikilia mpango wa kuwaondoa majeshi ya Marekani ifikiapo Agosti 31,Ujerumani ikitarajiwa kukamilisha shughuli za uokoaji ifikiapo Ijumaa 27 Agosti.
Chansela Angela Merkel wa Ujerumani amesema wanaweza kuendelea na shughuli za uokoaji ila kwa ushirikiano na serikali ya Marekani.
Marekani hadi sasa imefaulu kuwahamisha takriban waafghan 4000 na familia zao wanaoshikilia pasipoti za Marekani.
Wiki iliyopita serikali ya Marekani iliiomba serikali ya Uganda kuwapahifadhi angalau kwa muda wakimbizi 2000. Takriban wakimbizi 51 kutoka Afghanistan wamewasili Uganda 25 Agosti na wanafunzi 250 watapata hifadhi nchini Rwanda ili waendelee na masomo yao.
Uganda ina idadi kubwa ya wakimbizi barani Afrika ikiwa ni takriban wakimbizi 1.4 milioni.