Zanzibar itaingia kwenye historia itakapokamilisha ujenzi wa jengo la ghorofa 70 ambalo litakuwa na huduma mbalimbali. Jengo hilo litakuwa la kwanza Afrika Mashariki na kati litajengwa katika kisiwa cha Chapwani Mjini Unguja ambapo litahusisha hoteli na maeneo mengine ya biashara.
Litafahamika kwa jina la Zanzibar Domino Commercial Tower ujenzi wake utagharimu kiasi cha dola bilioni 3 sawa na shilingi za Kitanzania bilioni 3.01, likiwa na urefu wa mita 385.Ujenzi wake utatumia mita za mraba zipatazo 370,000 huku sehemu kubwa ya mchanga utakaotumika unatarajiwa kutoa bara ambapo tani 35,000 zitasafirishwa.