Ushauri kwa Watanzania waishio Ukraine

Februari 22, 2022 Ubalozi wa Tanzania, Stockholm ulitoa taarifa ya tahadhari juu ya uvumi uliokuwa unaendelea huko Ukraine juu ya uwepo wa Vita.

Wakati Ubalozi huo ukitoa tahadhari hiyo, hali hii leo imekuwa mbaya zaidi huku mashambulizi yakiendelea kati ya Ukraine na Urusi licha ya wito kutolewa kusitisha mashambulizi hayo ambayo yamegharimu maisha ya watu ambapo hadi sasa taarifa zinaeleza kuwa takribani watu saba wamepoteza maisha

Katika taarifaa hiyo iliyotolewa na ubalozi wa Tanzania ulieleza kuwa 

Kwa kuzingatia kuendelea kuwepo kwa hali tete ya kiusalama ambayo inasababisha baadhi ya Watanzania waishio Ukraine kuwa na mashaka juu ya usalama wao, ubalozi unawashauri wale wote ambao wanadhanai kuka kwao Ukraine siyo muhimu kwa sasa waondoke nchini humo.

Aidha kwa wale wazazi wenye watoto wanaosoma nchini humo na wanataka watoto wao warejee nyumbani kwa muda hadi hapo uvumi wa kutokea vita utakapoisha, tunawashauri wafanye taratibu binafsi za kuwarudisha watoto wao nyumbani kwa kutumia ndege za abiria zinazofanya safari kutokea Ukraine.

Tunashauri pia wanafunzi wote wanaotaka kurejea nyumba wahakikishe wanawasiliana na uongozi wa vyuo wanavyosoma na kukubaliana utaratibu wa kuendelea na masomo kwa nia ya mtandao kipindi chote watakapokuwa nje ya Ukraine