Notice: Function _load_textdomain_just_in_time was called incorrectly. Translation loading for the wordpress-seo domain was triggered too early. This is usually an indicator for some code in the plugin or theme running too early. Translations should be loaded at the init action or later. Please see Debugging in WordPress for more information. (This message was added in version 6.7.0.) in /home/mwanzotv/public_html/wp-includes/functions.php on line 6114
Mrema aoa kwa mahari ya milioni 4, alipa milioni 1 - Mwanzo TV

Mrema aoa kwa mahari ya milioni 4, alipa milioni 1

Mwenyekiti wa chama cha Tanzania Labor Part (TLP), Augustino Mrema leo Alhamisi Machi 24, 2022 amefunga ndoa na Doreen Kimbi katika kanisa Katoliki Parokia ya Uwomboni Kiraracha mkoani Kilimanjaro.

Mke wa mzee Mrema anayejulikana kwa jina la Doreen Kimbi amesema kuwa atamrudisha mzee Mrema ujanani.

“Mpaka kufikia hivi alivyo nimemfanya hivi. Katika kipindi cha uchumba nimemweka kuwa sawa, vitu vyote anavyohitaji anavipata. Kwa sasa amebadilika, nimeamua mwenyewe na sijashurutishwa na mtu na watarajie kuona anapendeza, nataka hadi awe kijana” amesema Doreen

Mzee Mrema amefunga ndoa na mwanadada huyo ikiwa ni takribani miezi sita tangu mke wake afariki dunia.

Amesema familia ya  Doreen ilimtaka alipie mahari ya  shilingi milioni 4.2 ambapo hadi sasa amelipa shilingi milioni 1.

Kumekuwa na taarifa kwamba huenda Doreen amekubali kuolewa na mzee mrema kwa sababu ya mali, taarifa hizo zinaelezwa kuwa ni za uongo baada ya Doreen mwenyewe kusema kwamba yeye hakwenda kwa Mrema kwa sababu yeye mwenyewe ni mwanamke anayejiweza kiuchumi.

“mimi si mwanamke wa kupewa, nimesimama mwenyewe na hata mali ninazo. Nilianza kujitafutia mimi, siendi kwake (Augustino Mrema) kutafuta mali. Lakini nikimlea vizuri akanipa mali si vibaya kwani ni mke wake.”

“Doreen ni mwanamke wa shoka, mpambanaji, siyo wale wa kupaka rangi na kucha ndefu, napenda kuchapa kazi, napenda kujisimamia na napenda kuwasaidia wanawake wenzangu,” amejinasibu.

Mrema ambaye kwa sasa ana miaka 77 aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini, kuwa mbunge na kugombea urasi wa Tanzania.