Mahakama kutoa uamuzi juu ya rufaa ya upande wa mashtaka dhidi ya shujaa wa ‘Hotel Rwanda’

Waendesha mashtaka wa serikali walikuwa wamekata rufaa dhidi ya hukumu ya awali, wakisema adhabu dhidi ya Paul Rusesabagina ni ndogo na inapaswa kuongezwa hadi kifungo cha maisha.

0
Paul Rusesabagina shujaa wa filamu ya ‘Hotel Rwanda’

Mahakama ya Rufaa ya Rwanda ilikuwa itatoa uamuzi Jumatatu juu ya rufaa ya upande wa mashtaka ili kuongeza kifungo cha jela dhidi ya shujaa wa “Hotel Rwanda” Paul Rusesabagina anayezuiliwa kwa tuhuma za ugaidi.

Mkosoaji mkali wa Rais Paul Kagame alihukumiwa kifungo cha miaka 25 jela baada ya kesi ambayo familia yake na wafuasi wake walidai kuwa ni kesi ya mchongo na uliyokumbwa na ukiukwaji wa sheria.

Waendesha mashtaka wa serikali walikuwa wamekata rufaa dhidi ya hukumu ya awali, wakisema adhabu dhidi ya meneja huyo wa zamani wa hoteli ya Kigali ni ndogo na inapaswa kuongezwa hadi kifungo cha maisha.

Jaji wa kesi ya awali alikuwa ameamua adhabu hiyo inaweza kupunguzwa hadi miaka 25 kwa sababu ilikuwa hukumu yake ya kwanza.

Upande wa mashtaka pia ulikata rufaa dhidi ya hukumu zilizotolewa kwa washtakiwa 20 wa Rusesabagina waliohukumiwa kifungo cha kati ya miaka mitatu hadi 20.

Washtakiwa wote walipatikana na hatia Septemba 2021 kwa kuunga mkono kundi la waasi wenye silaha linalodaiwa kuhusika na mfululizo wa mashambulizi mabaya nchini Rwanda mwaka wa 2018 na 2019.

Rusesabagina mwenye umri wa miaka 67 amesusia kesi ya kukata rufaa, huku familia yake ikisema hatashiriki “katika rufaa ya kupangwa.”

Rusesabagina anasifiwa kwa kuokoa maisha ya wzaidi ya watu 1,200 wakati wa mauaji ya kimbari ya 1994, ambapo 800,000 wengi wao wakiwa Watutsi lakini pia Wahutu wenye msimamo wa wastani waliuawa.

Lakini, katika miaka kadhaa baada ya Hollywood kumfanya kuwa mtu mashuhuri wa kimataifa, taswira tata zaidi iliibuka ya mkosoaji shupavu wa serikali ambaye hasira zake dhidi ya Kagame zilimfanya achukuliwe kama adui wa serikali.

Mwezi uliopita Kikosi Kazi cha Umoja wa Mataifa kuhusu vizuizi holela kilitoa maoni na kuhitimisha kwamba Rusesabagina “alitekwa nyara” alipokamatwa Agosti 2020 na kwamba kuzuiliwa kwake kulikuwa “kiholela” na kutaka aachiliwe mara moja bila masharti.

Familia ya Rusasabagina ambao tayari wameonya kuwa anaweza kufa gerezani — mwanzoni mwa Machi walisema afya yake ilikuwa imedhoofika na kwamba alihitaji matibabu mara moja. “Rusesabagina anaonekana kupata ulemavu wa sehemu ya uso ambao unadhoofisha usemi wake,”ilisema taarifa ya familia yake.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted