Kanuni mpya ya kikokotoo ambayo imetangazwa leo inaongeza kiwango cha mkupuo kutoka asilimia 25 iliyokataliwa mwaka 2018 hadi asilimia 33 kwa zaidi ya wanachama milioni 1.3 sawa na asilimia 81 ya wananchama wote wa mifuko ambao ni milioni 1.69.
Akizungumza leo Mei 26, 2022 Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Prof Jamal Katundu, amesema kikokotoo hiki pia kinaongeza pensheni ya mwezi kutoka asilimia 50 ya sasa hadi asilimia 66 kwa waliokuwa wanachama wa PSPF na LAPF ambao ni asilimia 19 ya wanachama wote wa mifuko ya hifadhi ya jamii.
Amesema mifuko ya pensheni ya NSSF na PSSSF itaimarika na kuwa endelevu na hivyo kuwa na uwezo wa kuongeza pensheni ya kila mwezi kwa kuzingatia tathmini zitakazo fanyika kila baada ya miezi mitatu