Asia Kibishe (27) mkazi wa Kijiji cha Nyarututu, Kata ya Bwanga, wilayani Geita amekutwa amejinyonga, huku chanzo kikidaiwa ni kutuhumiwa kuiba shilingi 10,000 ya mumewe.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Geita, Kamishna Msaidizi (ACP), Henry Mwaibambe amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, mapema mwezi huu saa 1;30 asubuhi.
Kamanda Mwaibambe amesema marehemu alikutwa amejinyonga kwa kutumia kipande cha kanga, ambapo marehemu mwili wake ulikutwa unaningâinia kwenye mti karibu na nyumbani kwao.
âChanzo cha tukio hilo ni mgogoro kati yake na mme wake aitwaye Fabian Shija (23), ambaye ni mkulima na mkazi wa kijiji hicho cha Nyarututu, kwamba alikuwa anamtuhumu marehemu kumuibia shilingi 10,000 iliyokuwa chumbani kwao,â amesema Kamanda huyo.
Pia amesema Jeshi la Polisi limsaka mtu mmoja kwa tuhuma za wizi wa mtoto aitwaye Evance Joseph, mwenye umri wa miezi sita na juhudi zinaendelea kumpata mtoto na mtuhumiwa.
âMnamo Septemba 3, 2022 majira ya saa saba mchana huko kijiji na kata ya Lulembela tarafa ya Ilolanguru wilaya ya Mbogwe, mama wa mtoto aitwaye Magreth Joel (23), aliripoti kuibiwa mtoto wake huyu,â amesema Kamanda.