Notice: Function _load_textdomain_just_in_time was called incorrectly. Translation loading for the wordpress-seo domain was triggered too early. This is usually an indicator for some code in the plugin or theme running too early. Translations should be loaded at the init action or later. Please see Debugging in WordPress for more information. (This message was added in version 6.7.0.) in /home/mwanzotv/public_html/wp-includes/functions.php on line 6114
Ahukumiwa kifugo cha maisha jela kwa kumnajisi mtoto wake wa kumzaa - Mwanzo TV

Ahukumiwa kifugo cha maisha jela kwa kumnajisi mtoto wake wa kumzaa

Mahakama ya Wilaya Tunduru mkoani Ruvuma, imemhukumu Mohamed Ngwelekwe (25) mkazi wa kijiji cha Namiungo, wilayani humo, kutumikia kifungo cha maisha jela kwa kosa la kumnajisi mtoto wake wa kiume wa kumzaa mwenye umri wa miaka minne.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Honorius Kando ambaye alisema, mtuhumiwa alitenda kosa hilo kwa nyakati tofauti katika kijiji hicho.

Alisema mtuhumiwa ametenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 158 kifungu kidogo cha(1)(a) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2019.

Hata hivyo, mtuhumiwa wakati akisomewa maelezo ya awali, alikiri kutenda kosa hilo na kuiomba Mahakama impunguzie adhabu.

Awali, kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, mtoto huyo ambaye jina lake limehifadhiwa alieleza kuwa kila alipokuwa anakataa kufanyiwa kitendo hicho ,baba yake alikuwa anamngā€™ata na kumpiga sehemu za mwili wake na kumtishia.

Shahidi mwingine ambaye ni daktari aliyemfanyia uchunguzi mtoto huyo, aliiambia Mahakama kuwa uchunguzi wa kitabibu umebaini ni kweli mtoto huyo alifanyiwa vitendo hivyo vya kinyama.

Mkuu wa wilaya ya Tunduru, Julius Mtatiro, alipongeza jeshi la polisi wilayani humo kupitia kitengo cha cha Dawati la Jinsia kwa jitihada walizofanya tangu serikali ilipopata taarifa hizo.

Mtatiro alisema, mtoto huyo amefanyiwa kitendo hicho kwa muda mrefu na kuwaasa wananchi popote walipo kutoa taarifa serikalini kila wanapobaini kuwepo kwa vitendo vya aina hiyo ambavyo ni kinyume na maadili na vina hatarisha ustawi wa kizazi cha sasa na kijacho.