Search
Close this search box.
Africa

Mahakama ya mkoa Manyara imemhukumu John Emmanuel (18) mkazi wa kijiji cha Malangi wilayani Babati kuchapwa viboko sita (6) baada ya kukutwa na kosa la ubakaji.

Hukumu hiyo ya kesi namba 73 ya mwaka 2021 imetolewa leo Septemba 26,2022 na Hakimu mkazi mkoa wa Manyara Mariam Rusewa.Hakimu Rusewa ameiambia mahakama hiyo kuwa Emmanuel alimbaka mwanafunzi wa darasa la nne (13) Septemba 10,2021 katika kijiji cha Malangi.

Kwa mujibu Kifungu cha 131 (2) cha sheria namba 16 kinaeleza kuwa, Bila kuathiri masharti ya sheria nyingine yoyote, ubakaji unapofanywa na mvulana wa miaka kumi na nane au chini; Kama mvulana huyo amefanya ubakaji kwa mara ya kwanza, atapewa adhabu ya viboko tu ambapo hakimu ataamua ni viboko vingapi.

Comments are closed