Search
Close this search box.
Africa

Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam linawashilia watuhumiwa wawili wakidaiwa kuhusika kwenye mauaji ya mwanamke mmoja ambayo yalitokea tarehe 1 Januari 2022.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Jumanne Murilo amesema tarehe 1 Januari kati ya watuhumiwa hao mtuhumiwa aliyefahamika kwa jina la Kassim Said Abdallah maarufu kama Bouncer, alimtongoza mwanamke aliyefahamika kwa jina la Bake Rashidi, mkazi wa mtaa wa Utete, wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kwenda nae hadi kwenye nyumba ya kulala wageni maeneo ya Tabata nyumba iliyofahamika kwa jina la Maridadi, Guest House.Lakini baadae majira ya saa 5 asubuhi, mwanamke huyu alikutwa akiwa amepoteza maisha.

Kamanda Murilo amesema, baada ya uchunguzi kufanyika kufuatia mauaji hayo ilibainika kuwa uchunguzi mwanamke huyo alikua ameuawa 

Mtuhumiwa Kassim Said Abdallah maarufu kama Bouncer, baada ya kufanyiwa mahojiano na polisi alikiri kutekeleza mauaji hayo, huku akidai kuwa alikodishwa na mwenzake ambaye ni mtuhumiwa wa pili aliyejulikana kwa jina la Charlse Gregory maarufu kama White kwa malipo ya pesa kiasi cha shilingi 1,700,000 na kabla ya kufanya mauaji hayo tayari alishalipwa shilingi 1,200,000 hivyo alikua anamdai shilingi 500,000.

Kwa mujibu wa Kamanda Murilo, chanzo cha mauaji hayo inadaiwa mtuhumiwa Chalrse Gregory au White, alikua ni rafiki wa karibu kimapenzi na marehemu na yeye alikua amegharamia sana ikiwemo kumpangishia nyumba lakini pia alikua akidai kwamba marehemu alikua na mapenzi na wanaume wengine.

Comments are closed