Aliyepandikizwa moyo wa Nguruwe afariki

Mtu wa kwanza kupandikizwa moyo wa Nguruwe amefariki dunia, miezi miwili baada ya kufanyiwa upasuaji huo katika hopsitali ya Maryland.

Machi 9,2022 hospitali hiyo ilitangaza kifo cha mtu huyo aliyefahamika kwa jina la David Bennett(57), ambapo katika taarifa yao ilieleza kuwa afya ya Bennett ilianza kudorora na kuwa mbaya siku kadhaa zilizopita.

“Alionekana kuwa mgonjwa jasiri ambaye alipigana hadi mwisho”alisema Dk. Bartley Griffith ambaye amemfanyia upasuaji marehemu Bennett.

David Bennett ambaye ni raia wa Marekani, alifanyiwa upasuaji huo wa upandikizaji moyo, mnamo January 7,2022 baada ya kugundulika kuwa ndio ulikuwa njia pekee ya matuamini ya kuokoa maisha yake.

Nguruwe aliyetumiwa katika upandikizaji huo alifanyiwa mabadiliko ya vinasaba ili kuondoa jeni kadhaa ambazo zingefanya kiungo hicho kikataliwe na mwili wa Bennet.

Madaktari waliofanya upandikizaji huo walisema mafaniko hayo yamehitimisha miaka kadhaa ya utafiti na yanaweza kubadili maisha duniani kote na ni hatua moja ya kukaribia kutatua mzozo wa ukosefu wa kiungo cha mwili.

Majaribio ya awali ya upandikizaji kama huo yalishindikana kwa kiasi kikubwa kwa huo yalishindikana kwa kiasi kikubwa kwa sababu miili ya wagonjwa ilikataa kiungo cha wanyama haraka