Ufikiaji wa mtandao yaani Internet katika nchi kadhaa za Afrika Mashariki ulikuwa wa kusuasua tangu siku ya Jumapili Mei 12, kutokana na nyaya za chini ya bahari kuharibika,
Pamoja na tatizo hilo kuikumba Afrika Mashariki yote lakini Tanzania na kisiwa cha Bahari ya Hindi cha Ufaransa cha Mayotte ndizo zilizoathirika zaidi.
Huduma nyeti za Internet zilisimama nchini Tanzania, huku waathirika wakubwa wakiwa ni wafanyabiashara wa mtandaoni wakiwemo madereva wa usafiri mtandao, wauza bidhaa, huduma za kibenki na kadhalika.
Katika ofisi nyingi za Umma na binafsi hakukua na huduma zilizohusiana moja kwa moja na matumizi ya mtandao ikiwemo Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ambao hapo jana Mei 13 uliutangazia umma kwamba Ubalozi huo umefungwa kwa siku mbili kutokana na ukosefu wa mtandao wa intaneti iliyoathiri nchi kadhaa za Afrika Mashariki.
Ubalozi huo umeahirisha miadi yote ya konsula kwa siku ya Jumanne na Jumatano hadi mambo yatakapotengamaa.
Tukio hilo limechangiwa na kushindwa kuathiri mifumo ya kebo ya SEACOM na EASSy chini ya bahari.
Waziri wa Habari na Teknolojia bwana Nape Nnauye aliuambia umma kwamba hitilafu hizo zilikuwa kwenye nyaya kati ya Msumbiji na Afrika Kusini huku akiwataka Watanzania kuwa wastahimilivu wakati ambapo utatuzi unafanyika kwa ushirikiano na mamlaka husika.
Mpaka hivi leo bado huduma ya mtandao maarufu kwa kimombo Internet haiko sawasawa na Serikali ya Tanzania kupitia Msemaji wake imesema bado haijajua ni lini huduma hiyo itarejea kwa uhakika.
Msumbiji na Malawi zilikuwa na athari za wastani huku Burundi, Somalia, Rwanda, Uganda, Comoro na Madagascar zikiwa na matatizo kidogo, NetBlocks ilisema.
Taifa la Afrika Magharibi Sierra Leone pia liliathirika.
Huduma zilikuwa zimerejeshwa nchini Kenya, NetBlocks ilisema lakini watumiaji wengi waliripoti muunganisho usio na waya.
Kampuni kubwa zaidi ya mawasiliano nchini Kenya Safaricom ilisema “imeanzisha hatua za kupunguza kazi” ili kupunguza kukatizwa.
“Hata hivyo, unaweza kupata kasi ya mtandao iliyopunguzwa,” iliwaambia watumiaji wake kwenye X.
Trafiki nyingi za mtandao duniani hupitia alama za nyaya za fiber optic zilizowekwa kando ya sakafu ya bahari, na mojawapo ya ndefu zaidi, ikiwa na kilomita 15,000 (maili 9,300), ikianzia Ureno hadi Afrika Kusini.
Mnamo mwaka wa 2009, SEACOM ilizindua nyaya za kwanza barani Afrika za nyuzi-optic zinazounganisha ukanda wa pwani ya mashariki na kusini, kulingana na tovuti yake.
Tukio hili si la kwanza, ilishawahi kutokea mara kadhaa katika miaka iliyopita lakini kwa mwaka huu ni tukio la tatu kutokea na inaelezwa kwamba matukio ya aina hii hutokea angalau mara 100 kwa mwaka
Nchi kadhaa za Magharibi na Kusini mwa Afrika zilikumbwa na matatizo kama hayo katikati ya mwezi Machi kwa sababu ya kuharibika kwa nyaya.
Intaneti ni mfumo mkubwa ambao mamilioni ya kompyuta na mifumo ya uendeshaji wa mfumo wa aina zote yanaweza kuwaunganisha. Hii ina maana ya mahusiano ya dunia yote pamoja.
Inakadiriwa kuwa hadi kufikia Juni 30,2009 watumiaji wa huduma ya Internet ilikuwa bilioni 1.67 duniani kote.
Tanzania tunapata huduma hii kupitia mikongo mitatu mikubwa yaani: 2Africa (inategemewa kuanza mwaka huu) Eastern African Submarine Cable System (EASSy) na SEACOM ambazo hizi ndio zimepata hitilafu;.