Ashikiliwa na Polisi kwa kuwapora watalii kisha kuwatelekeza

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi linamshikilia mtu mmoja kwa tuhuma za kuwapora watalii kisha kuwatelekeza huko Mombasa Wilaya ya Magharibi B” Mkoa wa Mjini Magharibi.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi ACP Richard ThadeI Mchomvu  alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Mohamed Aboud Mtoro (37), msukuma wa Darajabovu mkoani humo ambae alipora watalii waliotokea nchini Poland. 

Mtuhumiwa huyo alifanya kosa hilo tarehe 23/07/2022 akiwa na gari yenye namba za usajili Z.761 GP aina ya Noah Vox ambayo ilitumikakuwabeba watalii hao kutoka Mkoa wa Kaskazini Unguja wakielekea Mkoa wa Mjini ambapo aliwapora mali zao na kuwatelekeza.