Search
Close this search box.
Africa

Ginasa Petro (30), Mkazi wa Bariadi mkoani Shinyanga,  amekutwa amekufa baada ya kunywa sumu ya panya siku moja baada ya kuachwa na mke wake, Sara Jeremia.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe amewaambia waandishi wa Habari kuwa Mwili wa Petro ulipelekwa katika Kituo cha Afya Kayenze Wilayani Nyang’hwale mkoani Geita kwa ajili ya uchunguzi.

Kamanda Mwaibambe amedai kuwa kutokana na mgogoro wa kifamilia mke wa marehemu aliamua kuondoka nyumbani kwake na Jan. 29, marehemu alijaribu kumfuata mkewe katika kijiji cha Igula wilayani humo lakini hakufanikiwa.

Baada ya kushindikana, alirejea kwake na Januari 30, akaamua kuchukua uamuzi wa kukatisha maisha yake,” alisema Kamanda Mwaibambe.

“Chanzo cha tukio ni mgogoro wa kifamilia ambapo mke wa marehemu aitwaye Sara Jeremia aliondoka nyumbani walikokuwa wanaishi huko Kakola-Shinyanga.

Ameongeza “Januari 29 mwaka huu, marehemu alimufuata mke wake ili arudi nyumbani waendelee kuishi, mke wa marehemu alikataa ndipo marehemu aliporudi nyumbani na kuchukua maamuzi hayo”.

Amesema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi zaidi wa tukio na mwili wa marehemu baada ya uchunguzi wa daktari ulikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya mazishi.

Comments are closed