Search
Close this search box.
Africa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, ACP Stella Mutabihirwa

Mfanyabishara na mkazi wa mtaa wa Kipondoda Wilayani Manyoni  mkoa wa  Singida, Sita John (45) amefariki dunia na mkewe kujeruhiwa baada ya kupigwa. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, ACP Stella Mutabihirwa amesema kuwa tukio hilo limetokea Jumamosi Machi 05, 2022 wilayani Manyoni, ambapo siku ya tukio mfanyabiashara huyo alienda mnadani kuuza gari yake shilingi milioni 15. 

“Lakini badala ya kupewa fedha, alipewa ng’ombe (idadi haijajulikana) na fedha kiasi. Watu hawa wanaotaka kujipatia fedha kwa njia ya mkato, hawakujua kwamba mfanyabiashara Sita alipewa ng’ombe na fedha kiasi,”amesema.

Kamanda Stella amesema kuwa mkewe alijeruhiwa na kitu chenye ncha kali wakati akijihami kwenye tukio hilo na baada ya kupata taarifa ya tukio hilo, Polisi ilifanya msako na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja ambaye familia ya marehemu ilimtambua.

Amesema watu hao walifanikiwa kupora fedha ambayo kiasi chake bado hakijafahamika.

“Upelelezi juu ya tukio hilo unaendelea ikiwa ni pamoja na mahojiano na mtuhumiwa aliyekamatwa ili kuwafahamu watu anaoshirikiana nao katika matukio ya wizina mauaji” amesema.

Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida limewtaka wananchi kuachana na vitendo vya kujitafutia mali kwa njia zisizo halali.

Comments are closed