Mahitaji ya gesi kwenye magari yaongezeka nchini Tanzania
Mkurugenzi wa Biashara ya Mafuta na Gesi kutoka TPDC Dkt. Wellington Hudson amesema, hivi karibuni kumekuwa na misururu mirefu ya magari kuingia kwenye vituo vya kujazia gesi baada ya kuwepo kwa idadi kubwa ya watumiaji huku kituo kimoja kikisitisha kutoa huduma kutokana na matengenezo.