Mfumo wa ununuzi wa Luku kuzimwa kwa siku nne nchini Tanzania
Shirika la Umeme Tanzania limesema Wananchi nchini humo hawataweza kununua umeme kwa njia ya Luku kwa muda wa siku nne, Agosti 22 – 25, 2022 kuanzia saa 4 usiku hadi saa 1 asubuhi kutokana na matengenezo kwenye kanzidata ya mfumo wa Luku.