Vijana wa Gen Z Kenya waanzisha chama chao cha kisiasa
Sura mpya inajitokeza katika siasa za vijana wa Kenya maarufu kama Gen Z. Chama cha kisiasa kinachoongozwa na vijana kilichopewa jina ‘47 Voices of Kenya Congress’, kimeingia rasmi kwenye uwanja wa siasa nchini humo.