Filamu ya Avatar: The Way of Water iliyoandaliwa na James Cameron, imethibitishwa kuanza kusambazwa kwenye platform za OTT (over the top), Leo Machi 28, itakuwa siku ya kwanza kwa filamu hiyo ambayo ni ya pili kufuatia filamu ya Avatar ya mwaka 2009. Filamu hiyo itaanza kusambazwa kwenye mifumo ya digitali baada ya kukaa sinema tangu Desemba 16, 2022. Inasemekana kuwa filamu hiyo itapatikana kwa watumiaji wa platform za Amazon Video, Apple TV, Vudu, na Movies Anywhere.
Akaunti rasmi ya Instagram ya Avatar ilitangaza tarehe ya kuunza kusambazwa kwa Avatar 2, ilinukuu, “Rudi Pandora wakati wowote ukiwa nyumbani kwako, kupitia mtandao tu siku ya Machi 28. Tazama zaidi ya masaa matatu ya maudhui ambayo hayakuwahi kuonekana hapo awali kwa kuifanya #AvatarTheWayOfWater kuwa sehemy sinema zako.”
Filamu hiyo, inayowashirikisha Sam Worthington, Jake, Kate Winslet, Stephen Lang Quaritch, na Zoe Saldana, ilitolewa kwenye sinema tarehe 16 Desemba 2022 na ilipokelewa vizuri na mashabiki wake baada ya kuisubiri kwa miaka kumi.
Filamu ya Avatar 2 inashika nafasi ya nne kimataifa kwa filamu zilizopata mapato ya juu zaidi katika historia baada ya “Avatar1” (dola bilioni 2.92), “Avengers: Endgame” ($2.7 bilioni) na “Titanic” ($2.19 bilioni)
Filamu ya Avatar 2, iliyoandikwa na James Cameron na kutengenezwa na Cameron na Jon Landau, ilichukua zaidi ya muongo mmoja kutoka, ambayo ni sehemu ya pili ya filamu ya Avatar 2009.
Studio za 20th Century ziliiachia filamu ya Avatar; They Way of Water katika lugha saba, zikiwemo; Kiingereza, Kihindi, Kitamil, Kitelugu, Kikannada, na Kimalayalam.
pia unaweza kusoma Shujaa wa “Hotel Rwanda” Paul Rusesabagina aachiliwa huru
Filamu hiyo pia ameigiza Sigourney Weaver, Cliff Curtis, Joel David Moore, CCH Pounder, Edie Falco, na Jemaine Clement.
Pata dondoo za habari za Afrika mashariki. Kwa habari za biashara, siasa, teknolojia na michezo, tembelea mwanzotv.com