Search
Close this search box.
Africa

Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema baadhi ya mikoa itakosa umeme leo Julai 13, 2022 kutokana na upungufu kwenye mitambo ya uzalishaji umeme.

Taarifa iliyotolewa na shirika hilo imesema kuwa, upungufu huo umesababisha jumla ya megawati 91 kutokua kwenye mfumo wa usafirishaji umeme hivyo baadhi ya maeneo yatakosa nishati hiyo kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 12 jiioni.

”Siku ya leo (Jumatano) baadhi ya maeneo kwenye baadhi ya mikoa nchini yanakosa huduma ya umeme kwa nyakati tofauti kuanzia majira ya saa 3 asubuhi hadi saa 12 jioni” iimesema taarifa hiyo na kuongeza

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ni kwamba jitihada zinafanyika ili kuweza kurejesha mifumo katika hali ya kawaida na watajeja wataarifiwa pindi hali ya huduma ya umeme itakapoimarika.

“Jitihada za kurekebisha hali hiyo zinaendelea na tutawataarifu wateja wetu pindi hall ya upatikanaji wa huduma ya umeme itakapoirnarika. Shirika linaornba radhi kwa usumbufu wowote unaojitokeza”

Hata hivyo taarifa hiyo haijaainisha ni mikoa ipi ambayo itakosa huduma hiyo.

Comments are closed