Search
Close this search box.
Africa

Jeshi la Polisi Mkoani Geita linamshikilia mzee aitwaye, Grevas Katemi (89) mkazi wa Nyamisebeyi, wilayani Biharamulo mkoani Kagera kwa tuhuma za kumwingilia kumbaka mjukuu wake wa miaka 20.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Geita, Henry Mwaibambe ameelezea tukio hilo wakati akiwasilisha taarifa ya matukio yaliyojitokeza na kuvuta hisia kwa jamii kwa kipindi cha mwezi Juni 2021 hadi Februari mwaka huu,

Amesema mtuhumiwa huyo anadaiwa kutenda kosa hilo Februari 6 mwaka huu, majira ya saa nane usiku ambapo alimwingili kimwili mjukuu wake aitwaye Grace Tano akiwa amelala.

Ni kwamba mnamo Februari tano 2022, Modesta Katemi (54) mkazi wa mtaa wa Magogo (mjini Geita alipigiwa simu) na baba yake mzazi (Grevas Katemi) akimtaka amutumie wajukuu zake wakamsaidie kazi za kwenye mgahawa.

“Ndipo wajukuu wawili ambao ni Grace Tano (20) na mdogo wake Elizabeth Tano waliruhusiwa na kuweza kufika siku hiyo hiyo hadi nyumbani kwa babu yao huko Biharamulo,” ameeleza.

Ameongeza “Ilipofika majira ya saa nane usiku babu huyo alimfuata mjukuu wake  Grace, mahali alipokuwa amelala na kuweza kubaka,”.

Ameeleza baada ya kutenda tukio hilo Mzee Katemi (Babu) alikataa wajukuu zake kutorudi kwa wazazi wao huku akiwataka kutotoa taarifa za tukio hilo kwa wazazi wao na endapo watasema basi lazima watakufa.

“Kwa hiyo watoto walikimbia kutoka Biharamulo kuja kwa mama yao anayekaa Magogo (Geita mjini) ndo wakamwambia, babu ametufanyia hivi na hivi.

“Lakini walificha, mama akashangaa mbona watoto wangu hawapo vizuri, kuna tatizo gani?, mtoto mmoja ndiyo akaanza kulia, aah mama tumeambiwa tukisema tutakufa, mama akasema hapana Mwenyezi Mungu ndiyo muweza wa yote,”.

Mwaibambe amesema baada ya kupokea taarifa kutoka kwa mama yao mzazi, Jeshi la Polisi liliweka mtego na kumkamata katika kata ya Runzewe wilayani Bukombe mkoani hapa.

Comments are closed