Binti wa Alexander Dugin ambaye ni mshauri wa Putini, na mwana itikadi kali wa Urusi aliye karibu na Rais Vladimir Putin, ameuawa katika mlipuko wa bomu kwenye gari nje kidogo ya jiji la Moscow
Kulingana na wanafamilia walionukuliwa na vyombo vya habari vya Urusi, Dugin mfuasi mkubwa wa mashambulizi ya Kremlin nchini Ukraine — ndiye aliyelengwa na mlipuko huo kwani binti yake aliazima gari lake dakika za mwisho.
Daria Dugina aliuawa kwa bomu lililowekwa kwenye Toyota Land Cruiser lilipolipuka alipokuwa akiendesha kwenye barabara kuu karibu na kijiji cha Bolshie Vyzyomy, takriban kilomita 40 (maili 25) nje ya Moscow, Kamati ya Uchunguzi ya Urusi ilisema katika taarifa.
Daria, mwandishi wa habari aliyezaliwa mwaka 1992 ambaye mwenyewe aliunga mkono mashambulizi hayo waziwazi, alifariki katika eneo la tukio na uchunguzi wa mauaji umefunguliwa.
Mnamo Julai Uingereza ilimweka kwenye orodha ya Warusi waliowekewa vikwazo kwa madai ya kueneza habari potofu mtandaoni kuhusu Ukraine.
Dugin, 60, wakati mwingine huitwa “Putin’s Rasputin” au “Ubongo wa Putin,” ni msomi wa Kirusi aliye na msimamo mkali sana.
Kwa muda mrefu ametetea kuunganishwa kwa maeneo yanayozungumza Kirusi katika himaya mpya kubwa ya Kirusi na aliunga mkono kwa moyo wote operesheni ya Moscow nchini Ukraine.
Aliwekwa kwenye orodha ya vikwazo vya Magharibi baada ya Urusi kutwaa Crimea mwaka 2014, hatua ambayo pia aliunga mkono.
Hakukuwa na madai ya mara moja ya kuwajibika kwa shambulio hilo.
Mshauri wa rais wa Ukraine, Mykhailo Podolyak alikanusha kuwa mamlaka ya Kyiv ndiyo iliyohusika na shambulio hilo.
“Kwa hakika Ukraine haina uhusiano wowote na mlipuko wa jana kwa sababu sisi si taifa la uhalifu,” alisema katika matamshi ya televisheni.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Urusi Maria Zakharova aliandika kwenye mtandao waTelegram kwamba “ikiwa nadharia ya Kiukreni itathibitishwa … na lazima idhibitishwe na mamlaka husika, itakuwa sawa na ugaidi wa serikali kwa upande wa serikali ya Kyiv.”