Search
Close this search box.
Africa

Bondia wa Afrika Kusini afariki dunia kutokana na jeraha la ubongo

16

Bondia wa uzani mwepesi Simiso Buthelezi, 24, alifariki dunia baada ya kuvuja damu kwenye ubongo kufuatia pambano lililofanyika mwishoni mwa juma mjini Durban, Boxing South Afrika (BSA) ilisema Jumatano.

Pambano la raundi 10 la Shirikisho la World Boxing Federation All-Africa dhidi ya Mwafrika Kusini Siphesihle Mntungwa Jumapili lilisitishwa na mwamuzi wakati Buthelezi alipoanza kurusha ngumi hewani wakati wa raundi ya mwisho.

Alikimbizwa hospitalini na kuwekwa katika hali ya kukosa fahamu baada ya kugundulika alikuwa anavuja damu kwenye ubongo, lakini alifariki Jumanne.

BSA iliongeza kuwa kutakuwa na ukaguzi huru wa kitabibu wa mkasa huo huku mkufunzi Bheki Mngomezulu akisema Buthelezi alikuwa mzima wa afya wakati wa maandalizi ya pambano hilo.

Comments are closed

Related Posts