Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023 yenye jumla ya shilingi Bilioni 54.1.
Katika bajeti hiyo, shilingi Bilioni 14.7 ni ya Makamu wa Rais ambapo ni matumizi ya kawaida, shilingi Bilioni 1.2 kwa ajili ya mishahara na shilingi Bilioni 13.4 ni kwa ajili ya matumizi mengine.
Bunge limeridhia Ofisi hiyo ipatiwe shilingi Bilioni 39.3 ambapo kati ya fedha hizo shilingi Bilioni 20.7 ni kwa ajili matumizi ya kawaida na shilingi Bilioni 18.6 ni matumizi ya miradi ya maendeleo.
Matumizi ya kawaida yanajumuisha shilingi Bilioni 3.3 mishahara ya Ofisi ya Makamu wa Rais, shilingi Bilioni 5.2 mishahara ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira na shilingi Bilioni 12.0 matumizi mengine.