Mwanaharakati Wa Kenya Aliyetoweka, Ndiang’ui Kinyagia, Apatikana Akiwa Hai
DCI ilimhusisha Kinyagia na chapisho la uchochezi lililosambaa kwenye mtandao wa X (zamani Twitter), likihamasisha maandamano ya Gen Z ya Juni 25. Picha hiyo ilibeba nembo ya taifa na ratiba ya shughuli za kisiasa, ikiwemo maandamano kuelekea Ikulu na uapisho wa “baraza la mpito”.