Ruto azuru Sudan Kusini kuzindua upya mpango wa amani wa ‘Tumaini’
Baada ya maendeleo na kutiwa saini kwa itifaki tisa mwezi Julai, Makamu wa Rais Riek Machar alitangaza kujiondoa kwenye majadiliano. Riek Machar anasalia kuwa mpinzani mkuu wa Rais Salva Kiir, ingawa wanafanya kazi pamoja katika serikali ya umoja na ya mpito iliyoundwa chini ya makubaliano ya amani ya mwaka 2018.