Waziri Mkuu afafanua utata wa huduma za matibabu kati ya Zanzibar na Tanzania Bara
Waziri Mkuu wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amefafanua mjadala ulioibuka hivi karibuni kuhusu upatikanaji wa huduma za matibabu kati ya Zanzibar na Tanzania Bara, akisisitiza kuwa ushirikiano uliopo kati ya mifuko ya bima ya afya ya pande mbili za Muungano unaendelea kuruhusu wananchi kupata huduma bila ubaguzi.