Wapiganaji wa M23 wachukua mji muhimu wa Walikale nchini DRC licha ya jaribio la kusitisha vita
Kuchukuliwa kwa mji wa Walikale wenye wakazi takriban 60,000 mwishoni mwa siku ya Jumatano kunashiria kwamba kundi hili la wapiganaji limefika sehemu ya mbali kabisa magharibi kutoka eneo lao la awali tangu lilipojitokeza mwaka 2012.