CHADEMA yasusia uchaguzi mdogo madiwani, yaitaka Serikali kuheshimu uamuzi wa Mahakama ya Afrika 

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimsema kuwa hakitashiriki katika uchaguzi mdogo wa madiwani kwenye kata 14 zilizopo katika Halmashauri 13 za Tanzania Bara zilizotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Katika taarifa iliyotolewa na CHADEMA imeeleza sababu za kutoshiriki uchaguzi huo ambapo imesema uchaguzi huo utasimimamiwa na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya jambo ambalo ni kinyume na uamuzi wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu uliotolewa Juni 13, baina ya Chacha Wangwe dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Chadema tunatangaza kuwa hatutashiriki katika uchaguzi mdogo wa madiwani uliotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.Tunaitaka Serikali na Tume ya Tiafa ya Uchaguzi kuheshimu uamuzi  wa Mahakama ya Afrika na kutekeleza uamuzi huo kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wowote nchini” imesema sehemu ya taarifa hiyo

Pamoja na hayo CHADEMA imeitaka Serikali kuharakisha mchakato wa kupatikana kwa Katiba Mpya itakayokuwa na Tume Huru ya Uchaguzi na mabadiliko mengine ambayo yataweza kusimamamia uchaguzi huru na wa haki.

Itakumbukwa kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania jana ilitangaza Uchaguzi Mdogo wa Udiwani katika Kata 14 za Tanzania Bara utakaofanyika tarehe 13 Julai mwaka 2023.

Mkurugenzi wa tume hiyo bwana Ramadhani Kailima alisema kwamba uchaguzi huo unafanyika baada ya kupokea taarifa kutoka kwa waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa.

https://mwanzotv.com/2023/06/14/nec-yatangaza-uchaguzi-mdogo-katika-kata-14-nchini-tanzania/