China imefunga jiji la viwanda la watu milioni tisa kwa usiku mmoja na kuripoti visa zaidi ya 4,000 vya virusi siku ya Jumanne, wakati mkakati wa taifa wa “zero-Covid” ukikabiliwa na wimbi la Omicron.
Mamlaka za afya nchini humo ziliripoti maambukizo mapya 4,770 nchini kote, ambapo idadi kubwa ikiwepo katika mkoa wa kaskazini-mashariki mwa Jilin, kama mji wa Shenyang katika mkoa jirani wa Liaoning uliamriwa kufungwa.
China imesonga haraka katika wiki za hivi karibuni ili kupinguza wimbi la virusi kwa kuchagua upimaji wa watu wengi na kufungwa kwa jiji lote.
Siku ya Jumamosi iliripoti vifo viwili vya Covid-19 ikiwa ni mara ya kwanza kwa mwaka huu.
Mamlaka imeonya juu ya hatari inayoletwa na ukuaji wa watu nchini humo huku ikijitahidi kusawazisha mzozo wa kiafya na mahitaji ya uchumi wa pili kwa ukubwa duniani.
Shenyang, ambapo ni sehemu ya viwanda vikiwemo vya kutengeneza magari BMW,kuliripotiwa kesi mpya 47 za virusi vya COVID-19 leo Jumanne, huku mamlaka ikiweka amri kwa kuwazuia wakazi kutoka ndani ya saa 48.
Wiki iliyopita Rais wa China Xi Jinping alisisitiza hitaji la “kupunguza athari” za janga hilo kwa uchumi wa Uchina, lakini pia aliwataka maafisa “kushikamana” na mbinu ya sasa ya Covid-19.