China yaunga mkono kutatua mgogoro wa Ukraine kwa mazungumzo

Televisheni ya taifa ya China CCTV imeripoti kuwa rais wa nchi hiyo, Xi Jinping, amemwambia mwenzake wa Urusi Vladimir Putin kwamba Beijing inaunga mkono Moscow katika juhudi za kutatua mgogoro wa Ukraine.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyoripotiwa na televisheni hiyo ya taifa, ni kwamba viongozi hao wamefanya mazungumzo hayo kwa njia ya simu.

Rais wa China katika mazungumzo hayo amesema kwamba hali mashariki mwa Ukraine imepitia mabadiliko ya haraka na China inaunga mkono Urusi na Ukraine kutatua suala hilo kwa mazungumzo