Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Dkt. Charles Kichere, leo March 27,2025 amesema deni la Serikali limeongezeka na kufikia Tsh.trilioni 97.35 kutoka Tsh. trilioni 82.25 katika mwaka wa fedha uliopita.
Ameyasema hayo leo alipokuwa akisoma ripoti yake aliyoiwasilisha leo kwa Rais Samia Suluhu Hassan katika Ikulu ya Magogoni kwa mwaka wa fedha 2023/24 ambapo amesema “Kufikia June 30,2024 deni la Serikali lilifikia Tsh. trilioni 97.35, kiasi hiki kimeongezeka kutoka Tsh. trilioni 82.25 kilichokuwa kimeripotiwa katika mwaka wa fedha 2022/2023 hii ni sawa na ongezeko la Tsh. trilioni 15.1 ambalo ni sawa na asilimia 18.36”
CAG amesema deni hilo linajumuisha deni la ndani na deni ambalo ni Sh. trilioni 31.95 na la nje Sh.65.40, hata hivyo amesema deni hilo ni himilivu.
“Deni hilo linajumuisha deni la ndani la Tsh. trilioni 31.95 na deni la nje la Tsh. trilioni 65.40, tathmini ya uendelevu wa deni la Serikali imebaini kuwa deni la Taifa bado ni himilivu”