Search
Close this search box.
East Africa

Dereva wa safari rally nchini Kenya Maxine Wahome, alishtakiwa kwa shambulio siku ya Jumatano kufuatia kisa kilichomhusisha mpenzi wake na dereva mwenzake Asad Khan. 

Wahome, 26, alijizolea sifa tele alipokuwa mwanamke wa kwanza Mkenya kushinda mbio za daraja la tatu za WRC Safari Rally mwezi Juni.

Alifikishwa kortini Nairobi na kuachiliwa kwa dhamana ya Ksh 100,000 pesa taslimu. 

Waendesha mashtaka, ambao walikuwa wameomba azuiliwe kwa wiki mbili, waliambia mahakama Wahome alimvamia mpenzi wake mwenye umri wa miaka 50 katika nyumba yao siku ya Jumatatu.

“Khan amelazwa katika kitengo cha utegemezi wa hali ya juu akiwa katika hali mbaya na majeraha makubwa kwenye kifundo cha mguu wa kulia,” mwendesha mashtaka wa serikali James Gachoka alisema.

Wahome amekanusha mashtaka hayo.

Familia ya Khan ilitoa ombi kwenye mitandao ya kijamii siku ya Jumanne, ikitoa wito wa kuchangia damu.

Comments are closed