Search
Close this search box.
Africa

DRC ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki

12

Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wameipitisha rasmi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuwa mwanachama ndani ya umoja huo uliokuwa unaundwa na nchi sita.

DRC imepitishwa leo Machi 29, 2022 katika mkutano wa 19 wa wakuu wa nchi wa EAC uliofanyika kwa njia ya mtandao chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta

Akitangaza rasmi Kenyatta amesema ni jambo la kihistoria kufanyika katika Ukanda wa Afrika Mashariki.

“Kukubaliwa kwa DRC kunaashiria tukio muhimu katika historia ya ushirikiano wa eneo hili!,” amesema Kenyatta.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inakuwa mwanachama wa saba wa kambi hiyo ya kikanda.

Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo iliyo na idadi ya watu wanaofikia milioni 90 na inayopakana na nchi tano za jumuiya, iliomba kujiunga na taasisi hiyo ya kikanda mnamo Februari, 2021.

Kulingana na mkataba wa kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo , nchi nyingine inaweza kujiunga  iwapo itaungwa mkono na nchi wanachama na iwapo nchi hiyo inayoomba itakuwa imetimiza masharti  ya uongozi bora, Demokrasia, utawala sheria, inayosheshimu haki za binadamu, na kwamba iwe jirani na mojawapo ya nchi  wanachama.

Comments are closed

Related Posts