Search
Close this search box.
Africa

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji nchini Tanzania(Ewura), Mhandisi Modeatus Lumato amesema Tanzania ni kati ya nchi zinazouza mafuta kwa bei ya chini kutokana na ruzuku ya Serikali.

Amesema mbali na ruzuku hiyo, hatua ya kuwa wananunua mafuta kwa pamoja imesababisha kushuka kwa bei licha ya kuwepo kwa changamoto zilizosababisha kupanda kwa nishati hiyo kama baa la Uviko 19 lililoitikisa dunia.

Akizunguka katika Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ewura, Mhandisi Lumato amesema Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi zenye bei ndogo ya mafuta ikilinganishwa na nyingine hasa za Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Kulinga na bei ya mafuta ya rejareja ya dizeli iliyotangazwa siku nane zilizopita kwa Dar es Salaam na Tanga kwa Novemba 2022,  imepungua kwa shilingi 31 na shilingi 34 kwa lita ikilinganishwa na bei hizo kwa mwezi Oktoba mwaka huu.

Pia bei ya rejareja ya mafuta ya petroli kwa Bandari ya Dar es Salaam ingeongezeka kwa shilingi110 kwa lita, hata hivyo, Serikali imetoa ruzuku ili bei iliyopo ya Oktoba 2022 isibadilike.

“Ruzuku ya Serikali imesababisha kupungua kwa bei hii ndio maana bei yetu ni ndogo ikilinganishwa na nchi nyingine za Afrika,” amesema Lumato.

https://mwanzotv.com/2022/11/02/bei-mafuta-yaendelea-kupungua-nchini-tanzania/

Comments are closed