Search
Close this search box.
Africa

Shirika la habari linalomilikiwa na serikali nchini China CCTV, limesema kuwa hakuna manusura ambao wamepatikana katika eneo ambalo ndege ya abiria ya China ilianguka jana ikiwa imebeba abiria 133.

Mabaki ya ndege yamepatikana katika eneo la ajali hiyo lakini hakuna yeyote aliyekuwemo ndani aliyepatikana hai.

 Ndege hiyo aina ya Boeing chapa 737-800 ilianguka karibu na mji wa Wuzhou jimbo la Guangxi ilipokuwa ikipaa kutoka Kunming, kusini magharibi mwa Yunnan, kuelekea mji wa Guangzhou katika pwani ya mashariki nchini humo. 

Rais wa China Xi Jinping aliamuru operesheni ya uokoaji kufanywa. Ametaka uchunguzi kamili ufanywe kubaini chanzo cha ajali hiyo na kuhakikisha usalama wa usafiri wa ndege nchini humo. 

Hiyo ndiyo ajali mbaya zaidi ya ndege kuikumba China kwa zaidi ya muongo mmoja. 

Comments are closed