Search
Close this search box.
Africa

Hakuna wagonjwa COVID-19 Zanzibar

12

Zanzibar imeeleza kuwa hivi sasa haina mgonjwa hata mmoja wa ugonjwa wa uviko19 ingawa haiwezi kusema ugonjwa huo umeisha visiwani humo kwa kuwa huzuka na kupotea.

Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi aliyasema hayo jana Februari 16, 2022 wakati wa mahojiano yake na waandishi wa habari, Ikulu Zanzibar ambapo pamoja na mambo mengine alizungumzia kuanza kutumika kwa teknolojia mpya ya kupima Uviko19 kwa muda mfupi kwa kutumia simu (EDE) pamoja na kurejea kwa safari za ndege za mashirika kutoka umoja wa falme za kiarabu (UAE). 

“Kwa Zanzibar sasa maambukizi yapo chini, kipimo cha ugonjwa ni kuangalia wagonjwa waliopo hospitali kwa sasa hatuna hata mmoja aliyelazwa. Kwa ufupi Zanzibar iko salama,” amesema Rais Mwinyi huku akisema kuwa kasi ya watu kuchanja chanjo ya Uviko19 ni ndogo kuliko Serikali inavyotamani. Alisema  Rais Dk. Mwinyi

Kwa upande wake Waziri wa Afya wa Zanzibar Nassor Mazrui amesema tangu Januari mwaka huu Zanzibar haijaripoti kisa kipya cha Uviko-19 kwa wakazi wala wageni lakini haitoshi kusema kuwa ugonjwa huo umeisha.

“Hatuwezi kutangaza kuwa maambukizi yameisha visiwani Zanzibar labda tukikaa kama mwaka hivi bila kuwa na kisa kipya, Kila mtu angetamani kutangaza kuwa ugonjwa huo umeisha kwake lakini ni mapema kusema,” amesema Mazrui

Comments are closed

Related Posts