Search
Close this search box.
Africa

Halima Mdee na wenzake ni wabunge halali wa bunge la Tanzania

13
Spika wa Bunge la Tanzania, Dk Tulia Ackson

Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson amesema wabunge 19 wa Viti Maalum wa chama cha Chadema waliopo bungeni wapo kihalali si haramu kama ambavyo wengine wanasema.

Dk. Tulia amesema anasubiri michakato halali ndani ya chama chao na ngazi zingine ikithibitika hakuna shida atatekekeza takwa la kikatiba, litakawaondoa ndani ya bunge hilo, kwani ili uwe mbunge ni lazima uwe mwakilishi wa chama fulani

Wabunge hao 19 ni Halima Mdee,  Grace Tendega, Ester Matiko, Cecilia Pareso, Ester Bulaya, Agnes Kaiza, Nuzrat Shaban Hanje, Jesca Kishoa, Stella Simon Fiao, na Hawa Mwaifunga.

Wengine ni  Felista Deogratius Njau, Nagenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunt Majala, Tunza Malapo, Asna Mohamed, Anatropia Theones, Salome Makamba na Conjesta Rwamulaza.

Novemba 2020 wabunge hao waliapishwa, jambo lililozua mjadala mkubwa juu ya namna walivyoteuliwa na majina yao kupelekwa Bungeni kwani chama chao hakikutoa ridhaa.

Spika Dk Tulia ametoa kauli hiyo leo Jumatatu februari 14, 2022 jijini Dodoma, wakati akizungumza na Wahariri na waandishi wa habari wanaoripoti Bunge.

Akijibu swali kuhusu uhalali wa wabunge wao, Spika amesema hadi sasa wabunge hao wapo kwa mujibu wa sheria kwani kila mbunge ni lazima atokane na chama na hao nao wametokana na chama.

Amesema Bunge halioni shida kuwaondoa wabunge na lilishawahi kufanya hivyo katika mabunge yaliyotangulia.

Comments are closed

Related Posts