Rais wa Ivory coast, Alassane Ouattara,na Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo walimtembelea kiongozi wa mapinduzi na junta Mamady Doumbouya,mjini Conakry kuomba kuachiliwa kwa Rais Conde. Rais Ouattara alitarajia kuondoka na Conde,afisa mkuu amesema.
“Aliyekuwa rais yupo na ataendelea kusalia nchini Guinea. Hatutakubali kushinikizwa kumuachilia.” Jeshi lilisema katika ripoti yake kwenye kituo cha televisheni ya kitaifa.
Rais Ouattara wa Ivory Coast, alikiambia kituo cha redio mjini Conakry
“Nimekutana na kakangu, Alpha Conde, yuko salama,anaendelea vyema. Na tutandelea kuwasiliana nae.”
Rais Nana Akufo-Addo alikiambia kituo cha televisheni RTG “Tumekuwa na mazungumzo ya wazi na Doumbouya na wenzake. Nafikiri ECOWAS na Guinea tutaendelea kutafuta suluhu ili tusonge mbele pamoja”
ECOWAS imeagiza kurudishwa kwa uongozi wa kikatiba tangu vikosi maalum vilipochukua uongozi wa nchi na kumzuia Conde.
Jumuia ya ECOWAS, ilizuia akaunti za benki za majeshi na familia zao na kuwazuia kusafiri kutoka Guinea.