Search
Close this search box.
Africa

Hukumu kesi ya Sabaya yaahirishwa

9
Lengai Ole Sabaya

Hukumu ya kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili iliyokuwa itolewe leo imeahirishwa hadi Oktoba 15, 2021. Sabaya na wenzake, Sylvester Nyegu na Daniel Mbura, wanakabiliwa na mashtaka matatu ya unyang’anyi wa kutumia silaha.

Inadaiwa katika shtaka la kwanza kuwa mnamo Februari 9, 2021 katika Mtaa wa Bondeni, jijini Arusha, washtakiwa hao
waliiba shilingi milioni 2.769, mali ya mfanyabiashara Mohamed Saad. Upande wa mashtaka ulidai kuwa kabla na baada ya kufanya wizi huo, washtakiwa waliwashambulia Numan Jasin, Harijin Saad Harijin, Bakari Msangi, Salim Hassan na Ally Shaban kwa kuwapiga kwa kutumia bunduki, ili kufanikisha wizi huo.

Katika shtaka la pili, Sabaya na wenzake wanadaiwa kuiba shilingi 390,000 kutoka kwa diwani wa Kata ya Sombetini, Bakari Msangi wakiwa katika Mtaa wa Bondeni. Walidaiwa kumfunga pingu, kumpiga na kumshambulia huku
wakimtishia kwa bunduki kabla ya kufanya tukio hilo.

Shtaka la tatu Sabaya na wenzake wanadaiwa kuiba shilingi 35,000 na simu ya mkononi aina ya Tecno kutoka kwa Ramadhan Rashid wakiwa katika mtaa huohuo. Baada ya kufanya wizi huo, walidaiwa kumfunga pingu na
kumtishia Rashid kwa bastola.

Awali kesi hiyo ilikuwa ikitajwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Salome Mshasha lakini kuanzia Julai 18, 2021 kesi hiyo ilianza kusikilizwa mfululizo na hakimu Odira Amworo aliyekuja Arusha
akitokea Geita.

HALI ILIVYOKUWA LEO MAHAKAMANI


Nje ya Mahakama, watu wengi wamejitokeza tofauti na siku za hivi karibuni wengi wakiwa na shauku ya kujua Sabaya na wenzake watahukumiwa nini.

Watu wameanza kufika mahakamani hapo mapema leo asubuhi kabla ya hata gari la mahabusu kuwasili.
Hukumu hiyo inatarajiwa kutolewa leo na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Odira Amworo baada ya
kusikiliza kesi dhidi ya Sabaya na wenzake wawili kwa miezi miwili na nusu iliyopita.

Comments are closed

Related Posts