,

Jaribio la Mauaji ya Trump: Kilichotokea

Joy Cheptoo Avatar

Donald Trump alinusurika kwa tundu la sindano katika jaribio la mauaji kwenye mkutano wa kisiasa Jumamosi. Shirika la upelelezi ya nchini Marekani (FBI) sasa inachunguza tukio hilo.

Kilivyotokea:

  • Trump, akiwa amevaa shati jeupe, koti jeusi, na kofia nyekundu ya MAGA, alikuwa akizungumza dhidi ya uhamiaji haramu wakati risasi zilipoanza kurindima saa 12:08 jioni.
  • Trump alishika sikio lake la kulia huku risasi nne zikifyatuliwa, ikifuatiwa na risasi ya tano na ya sita.
  • Maajenti wa Secret Service walimzunguka Trump haraka huku akiinama nyuma ya mimbari.
  • Risasi zaidi zilifyatuliwa, zikisababisha hofu kwa umati.
  • Ndani ya sekunde 22, vikosi vya usalama vilipanda jukwaani na Trump aliinuliwa na maajenti.
  • Trump aliwahakikishia umati yuko salama, akaongozwa kutoka jukwaani, akasindikizwa hadi kwenye gari la usalama.

Jibu la Trump:

  • Trump alichapisha kwenye Truth Social saa 2:42 usiku, akisema alipigwa risasi na kuhisi risasi ikipenya sikio lake la kulia.
  • Rais Joe Biden alifahamishwa na kulaani tukio hilo, akikatisha mapumziko yake ya ufukweni kurudi Washington.

Mshambuliaji Alitambulika:

  • FBI ilimtambulisha mshambuliaji kama Thomas Matthew Crooks, kijana wa miaka 20 kutoka Bethel Park, Pennsylvania.
  • Crooks, aliyesajiliwa kama Republican, aliwahi kuchangia dola 15 kwa kundi la wapiga kura wa mrengo wa kushoto.
  • Mshambuliaji alipiga risasi kutoka juu na alidhibitiwa na maajenti.

Waathiriwa:

  • Mshambuliaji na mshiriki mmoja waliuawa; watazamaji wawili walijeruhiwa vibaya.
  • Mashuhuda waliripoti kumuona mtu aliyepigwa risasi kichwani na mwanamke mwingine aliyepigwa risasi mkononi.

Polisi wa eneo hilo walijibu ripoti za shughuli za kutiliwa shaka lakini hawajatoa maelezo zaidi.

Our Correspondent Avatar