Jeshi la Polisi Tanzania lawaondoa hofu wananchi juu ya taarifa ya Ubalozi wa Marekani 

Jeshi la Polisi Tanzania limewaondoa hofu Wananchi kufuatia taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Marekani nchini humo, iliyoeleza kuwepo kwa uwezekano wa kutokea uhalifu wa kigaidi.

Taarifa iliyotolewa leo January 26,2023 kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi imeeleza kuwa hali ya ulinzi na usalama ni shwari kwani matukio makubwa yanayoweza kuleta hofu kwa Wananchi yanaendelea kudhibitiwa.

Hata matukio yale ambayo yametokea yanaendelea kushghulikiwa na wahalifu wanaendelea kukamatwa. Aidha Jeshi la Polisi linaendelea na mikakati yake kuhakikisha tunabaini na kuzuia uhalifu kwa kiwango kikubwa zaidi kwa mwaka huu 2023” ilisema sehemu y taarifa hiyo

Taarifa hiyo pia imeeleza mikakati iliyowekwa kwa ajili ya kukabiliana na matukio ya uhalifu nchini amabapo ni kutoa elimu kwa jamii lengo likiwa ni kuwajengea uwezo Wananchi ili wawe karibu zaidi na Jeshi la Polisi katika kubaini na kuzuia uhalifu kuliko kusubiri utokee.

Jana Januari 25,2023 Ubalozi  wa Marekani nchini Tanzania ulitoa taarifa kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ikiwemo mtndao wa Twitter, ikitoa tahadhari kwa wananchi wao waliopo hapa nchini wakiwatahadharisha uwezekano wa kutokea uhalifu wa kigaidi maeneo yanayopendwa kutembelewa na watu wengi hapa Tanzania wakiwepo wageni wengi kutoka nchi zingine.

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi iliyotolewa leo mara baada ya kuipata taarifa hiyo ya Ubalozi wa Marekani walianza kufanyia kazi na kwamba  Wananchi waendelee kuwa watulivu na kuendelea na shughuli zao kama kawaida.