Ofisa Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba SC, Ahmed Ally amesema kabla ya Februari 18, 2023 mzigo wa jezi mpya utakuwa umefika Tanzania ukitokea Ethiopia ambako umekwama.
Akizungumza leo Februari 15, 2023 Ahmed Ally amesema jezi hizo zilianza kukwama nchini China hivyo zilifanyika juhudi za kusukuma mzigo huo ili kuachiwa kwa haraka na baada ya kuachiwa ukakwama tena Ethiopia.
“Kutokana na sherehe za mwaka mpya China usafirishaji mizigo ulikuwa wakusuasua ikabidi Vunjabei aende China kuhakikisha jezi hazichelewi ila zikaja kukwama Ethiopia kwasababu ya ndege za mizigo kuchelewa.” Amesema Ahmed Ally.
Amesema kuwa kabla ya mchezo wa pili wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Raja Casablanka jezi hizo zitakuwa zimefika na kila shabiki atakapata kutokana uwingi wa jezi hizo.