JWTZ yawaonya wanaotumia sare zao, wataka wajisalimishe.

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetoa siku saba kwa wananchi kusalimisha mavazi ya jeshi au yanayofanania na sare za jeshi hilokuanzia leo Agosti 24, 2023, kwa kuwa ni kinyume na sheria.

Kaimu Mkurugenzi wa habari na uhusiano Makao Makuu ya Jeshi (JWTZ) Luteni Kanali Gaudentius Ilonda ametoa kauli hiyo Leo Jijini Dodoma mbele ya wanahabari, ambapo amesema katazo hilo la mavazi ni kwa mujibu wa kifungu cha 99 cha sheria ya Ulinzi wa Taifa (NDA) Sura ya 192 sheria namba 24 ya mwaka 1966 iliyofanyika marejeo mwaka 2002.

“Zipo baadhi ya taasisi zinazowashonea watumishi wake sare za aina hiyo. Wapo pia wafanyabiashara wanaoingiza nchini mavazi ya aina hiyo na kuyauza kwa baadhi ya raia katika maduka au maeneo yao ya biashara. Wapo baadhi ya wasanii wanaovaa mavazi hayo na kuyatumia wawapo kwenye majukwaa ya kazi zao bila kufuata utaratibu,” amesema.

Luteni Kanali Ilonda amesema wapo baadhi ya watu ambao kwa kuyatumia mavazi hayo wamekuwa wakiwatapeli wananchi na wengine kufanyae vitendo viovu ambao piae wamekuwa wakidhaniwa kuwa nie Wanajeshi, vitendo hivyo ni vya uvunjifu wa sheria za nchi na havipaswi kufumbiwa macho na halie hiyo ikiachwa inaweza kuhatarisha ulinzi na usalama wa nchi.

“Siyo hekima kwetu kulumbana kwa namna yoyote ile na baadhi ya wananchi wenye mavazi yaliyokatazwa. Ndio maana tunatoa siku saba kuyasalimisha bila kuchukuliwa hatua ili kuepuka usumbufu, ambaye hatayawasilisha atakuwa na nia ovu na mbaya,” ameongeza.

Aidha Luteni Kanali Ilonda amesema Jeshi la Wananchi Tanzania linawasihi na kuwaomba Wananchi kusalimisha mavazi hayo ndani ya siku Saba (7) na baada ya siku hizo Saba atakayekutaa na mavazi hayo atachukuliwa hatua za kisheria“Mahusiano ya Jeshi letu na wananchi ndiyo mhimili mkubwa ndani ya nchi na nje ya nchi, sio hekimae kwetu kulumbana kwa namnae yoyotee Ile na baadhie ya wananchi wenyee mavazie yaliyokatazwa ndiyo maana tunatoa siku sabae kuyasalimisha bila kuchukuliwa hatuae ili kuepukae usumbufu kwa ambayee hatayawasilisha atakuwa na nia ovu na dhamira mbaya” imesema sehemu ya taarifa hiyo.