Rais wa Kenya William Ruto alisema jana kuwa wafugaji wa kaskazini hawataruhusiwa tena kubeba silaha wakati wanachunga ng’ombe wao huku kukiwa na operesheni ya kuwapokonya silaha.
“Kuanzia sasa, hakuna mtu atakayeruhusiwa kuchunga akiwa na silaha. Silaha ni za maafisa wa usalama tu,” gazeti la Kenya lilimnukuu Ruto.
Msamaha wa kusalimisha bunduki kwa hiari kaskazini mwa nchi hiyo ulikwisha tarehe 21 Februari na 19 pekee bunduki zilipatikana.Serikali inakadiria kuwa maelfu ya silaha zinashikiliwa na raia.
Wanajeshi na polisi wanaendesha operesheni katika kaunti 10 hivi maeneo ya kaskazini, ambapo wizi wa ng’ombe unaochochewa na kuenea kwa bunduki haramu umesababisha ukosefu wa usalama kwa miaka mingi.
Ruto pia alisema serikali itawekeza $156.4m kununua vifaa vya kupambana na ugaidi na uhalifu mwingine.