Kenya imetangaza Jumatano, Aprili 10, 2024 kuwa siku kuu kuadhimisha Eid-Ul-Fitr. Eid-ul-Fitr ni sikukuu kwa Waislamu ambayo inaashiria mwisho wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan ambao ni wa tisa wa kalenda ya Kiislamu.
Tangazo hilo lilichapishwa katika gazeti rasmi la serikali na waziri wa usalama kenya Prof Kithure Kindiki siku ya Jumanne asubuhi.
“Katika kutekeleza mamlaka yaliyotolewa na kifungu cha 2 (1) cha Sheria ya Sikukuu za Umma, natangaza Jumatano, Aprili 10 2024, itakuwa sikukuu ya kuadhimisha Idd-ul-Fitr,” Waziri wa usalama nchini Kenya Kithure Kindiki alisema.
Sherehe hiyo huanza kwa sala maalum, inayojulikana kwa jina la Eid, inayoswaliwa mapema asubuhi baada ya kuonekana kwa mwezi.