Search
Close this search box.
Africa

Kesi ya Wanavijiji wa Loliondo dhidi ya Waziri wa Utalii na Maliasili, waleta maombi wapewa siku 14 kuleta maombi yao.

13

Shauri No 9 ya mwaka 2022 kuhusu maombi ya mapitio ya Sheria (Judicial Review Application) dhidi ya tangazo la Waziri wa Mali asili na Utalii (GN no 421 ya tarehe 17 Juni 2022 kuhusu ardhi ya vijiji vya Loliondo kuwa pori tengefu la Pololeti ,limetolewa jana Novemba 16 2022 ambapo waleta maombi wamekubaliwa kuleta maombi yao ya msingi ndani ya siku kumi na nne(14) baada ya Mahakama kujiridhisha kwamba waleta maombi wana Msilahi,Wako ndani ya muda na pia kesi yao ina mashiko .

Uamuzi huo ulitolewa mawakili Jebra Kambole na Wakili Denis Moses Oleshangai kwa niaba ya waleta maombi na kwa upande wa Serikali alikuwepo wakili Zamaradi Johanes.

Katika shauri hilo Waleta maombi watano kutoka vijiji vilivyoathirika wanaomba Mahakama:

1) Iagize Serikali kuondoa zuio dhidi ya Wananchi kuingia kwenye eneo la Km2 1500 ambalo wamekuwa wakitumia kwa ajii ya malisho ya mifugo yao na kwa ajili ya kufanyia shughuli za imani yao

2) Mahakama itamke kwamba Tangazo la Serikali (GN421) la tarehe 17 Juni 2022 ni Batili na lisitumike kwani ni kinyume na sheria na pia haikuwashirikisha wananchi kama sheria inavyotaka.

3) Mahakama itamke kuzuia Serikali na Mawakala wake wasifanye oparesheni zote kwenye eneo hilo

Comments are closed

Related Posts