Kiongozi wa upinzani nchini Msumbiji agoma kujiunga na Serikali Mpya

Kiongozi wa upinzani nchini Msumbiji, Venancio Mondlane,amesema hatajiunga na serikali mpya iliyoundwa baada ya mzozo wa miezi kadhaa kuhusu matokeo ya uchaguzi. 

Mondlane, ambaye alidai kushinda uchaguzi wa urais wa Oktoba na kudai kuwa matokeo hayo yalichakachuliwa, alisema yuko tayari kusaidia kutafuta suluhu lakini “sio kuwa sehemu ya serikali.”

Daniel Chapo alishindwa kuwa rais wiki moja iliyopita, akiwaahidi kuleta umoja nchini baada ya ghasia za uchaguzi zilizochukua maisha ya takriban watu 300.

Mondlane ameitisha maandamano mapya ili kuunga mkono madai yake kuwa uchaguzi huo ulinyakuliwa na kutoa “masharti” kwa serikali kwa ajili ya amani.

Alisema kuwa hajawahi kuzungumza na Chapo ili kumaliza mzozo huo. “Daniel Chapo na mimi hatujawahi kuwa na mawasiliano ya moja kwa moja. Hatujawahi kuwa na mawasiliano ya moja kwa moja,” alisema.

Mondlane anahusisha chama cha Frelimo cha Chapo na ulaghai katika uchaguzi huo. Alirudi kutoka uhamishoni kwa hiari tarehe 9 Januari na kusema kuwa yuko tayari kujadiliana ili kumaliza mzozo huo.

“Nina seti ya masharti ya awali ambayo naamini ni muhimu kwa mwongozo wa amani na maridhiano.Kama katika miezi mitatu ijayo, wataweza kujibu maswali ambayo ni muhimu kwa watu, sina shida kushirikiana na serikali. Lakini si kuwa sehemu ya serikali – sitaki. Nimesema mara kadhaa kwamba sitaki kuwa sehemu ya serikali,” alisisitiza.